The Orange Door

Kiswahili

Habari katika Kiswahili

The Orange Door hutoa usaidizi na msaada kwa unyanyasaji wa familia, pamoja na familia zinazohitaji usaidizi wa ustawi na maendeleo ya watoto.

Wakati fulani mambo ya nyumbani au katika uhusiano si SAWA na unahitaji msaada na usaidizi. The Orange Door iko hapa ili kukusikiliza na kukusaidia kupata usaidizi unaohitaji haraka na kwa urahisi.

Ikiwa uko katika hatari ya haraka, piga Sifuri Tatu (000).

The Orange door inaweza kusaidia kama:
 • Unahitaji usaidizi katika malezi, au una wasiwasi kuhusu ustawi au ukuaji wa mtoto au kijana.
 • Mtu wa karibu na wewe anakufanya ujisikie kuwa na hofu au huna usalama kama vile mpenzi wako, mpenzi wako wa zamani, mwanafamilia au mlezi.
 • Wewe ni mtoto au kijana ambaye hujisikii salama au kutunzwa.
 • Uko katika hatari ya kutumia tabia ya matusi au kudhibiti au unahitaji usaidizi wa tabia hizi nyumbani au katika uhusiano.
 • Una wasiwasi juu ya usalama wa mtu  unayemjua.
 • Umepitia vurugu za familia, ikiwa ni pamoja na kudhibiti tabia kama vile mtu anayefuatilia unakoenda, unayemtembelea au jinsi unavyotumia pesa.

The Orange door inaweza kusaidia kwa:
 • Kukusikiliza na kusikia wasiwasi wako unahusiana na nini.
 • Kufanya kazi na wewe ili kutambua usaidizi na msaada unaohitaji.
 • Kukusaidia kwa ustawi na maendeleo ya watoto na vijana.
 • Kukusaidia kufanya mpango wa usalama ili kukuweka wewe na watoto wako salama.
 • Kukuunganisha kwenye huduma zinazoweza kukusaidia, kama vile ushauri nasaha, malazi, usaidizi wa unyanyasaji wa familia, afya ya akili na huduma za dawa za kulevya na pombe, vikundi vya usaidizi wa wazazi, huduma za watoto, usaidizi wa kifedha, au usaidizi wa kisheria.
 • Kukusaidia kupata ufadhili wa gharama za kimsingi za maisha na gharama zingine.
 • Kufanya kazi na wewe ili kukusaidia kubadilika ikiwa unatumia tabia ya matusi au kudhibiti nyumbani au katika uhusiano.

Ninawezaje kupata The Orange Door?
The Orange Door inafunguliwa saa 3 asubuhi (9am) hadi saa 11 jioni (5pm) Jumatatu hadi Ijumaa (hufungwa wakati wa likizo za umma).

Tafuta kulingana na sehemu au namba ya posta ili kutafuta huduma ya mahali.

The Orange Door inaweza kufanya kazi nawe ikiwa unatumia vifaa vya mawasiliano au unahitaji mkalimani, ikiwa ni pamoja na Auslan.

Nahitaji mkalimani
Julisha huduma ikiwa unahitaji mkalimani. Julisha huduma ili ijue:
 • namba yako ya simu
 • lugha yako 
 • wakati ambao ni salama kuweza kupiga simu. 

 Kisha mkalimani atakupigia simu tena. 

Je, The Orange Door ni huduma iliyoundwa kwa ajili yangu?
The Orange Door inakaribisha watu wa umri wowote, jinsia, ujinsia, utamaduni, na uwezo. Mapendeleo yote ya kitamaduni na kidini yanaheshimiwa. Mjulishe mfanyakazi ikiwa unapendelea kufanya kazi na mfanyakazi wa kiume au wa kike. The Orange Door hufanya kazi na huduma za kitamaduni, huduma za LGBTI na huduma za walemavu ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya watu binafsi na familia. Wafanyakazi watakupa taarifa kuhusu chaguo na kukuunganisha kwenye huduma unazohitaji.

Ikiwa wewe ni mhamiaji au mkimbizi au huna ukaaji wa kudumu, bado tunaweza kukusaidia. Usiogope kutafuta usaidizi kwa sababu ya hali yako ya uhamiaji. Hii ni huduma ya bila malipo. Julisha wafanyakazi wa The Orange Door ikiwa ungependa kujadili hali yako kwa simu au ana kwa ana.
Je, niende wapi wakati The Orange Door haijafunguliwa?  
Wasiliana na huduma zifuatazo nje ya saa hizi:
 • Huduma ya Rufaa ya Wanaume kwa 1300 766 491 (8am-9pm Jumatatu-Ijumaa na 9am-6pm Jumamosi na Jumapili na Likizo za Umma) (Ushauri wa simu kwa unyanyasaji wa familia ya wanaume, habari na huduma ya rufaa)
 • Safe Steps ni huduma ya usaidizi kwa waathiriwa wa unyanyasaji wa familia 1800 015 188 (saa 24, siku 7 kwa wiki). Unaweza pia kutumia Safe Steps barua pepe au kutumia huduma yao ya usaidizi ya zungumzo la moja kwa moja la wavuti
 • Victims of Crime Helpline (Nambari ya usaidizi ya Waathiriwa wa Uhalifu) (kwa waathiriwa wote wa uhalifu na waathiriwa wa kiume wazima wa unyanyasaji wa familia) 1800 819 817 au tuma SMS kwa      0427 767 891 (8am-11pm, kila siku)
 • Sexual Assault Crisis Line (Laini ya Mgogoro wa Unyanyasaji wa Ngono ni kwa ajili ya waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia) 1800 806 292 (saa 24, siku 7 kwa wiki)

Ikiwa wewe au mtu mwingine yuko katika hatari ya haraka, piga simu Sifuri Tatu (000) kwa usaidizi wa dharura.  

Maoni na faragha
Unaweza kutoa maoni kuhusu matumizi yako na The Orange Door kwa kutumiafomu ya maoni ya kwenye mtandao kwenye orangedoor.vic.gov.au/feedback au kwa kupiga simu 1800 312 820 na kuomba kuzungumza na mfanyakazi wako, msimamizi au meneja.

Tunachukua faragha yako kwa umuhimu kabisa. Ili kujua jinsi tutakavyotumia maelezo yako, tafadhali rejelea kwenye sera yetu ya usiri.